← Volver
Libros

Mwanamke na Uzao

by Mch. Joyce Nkone

Written by Mch. Joyce Nkone for women searching for their own worth. Beginning from the truth that woman was made in the image and likeness of God, it confronts self-doubt and comparison, traces the enmity set between the woman and the serpent, and points toward the calling and the seed entrusted to her.

$6.99 ≈ TSh15,000
Mwanamke na Uzao
Written by Mch. Joyce Nkone for women searching for their own worth. Beginning from the truth that woman was made in the image and likeness of God, it confronts self-doubt and comparison, traces the enmity set between the woman and the serpent, and points toward the calling and the seed entrusted to her.
Muestra gratuita

Lee los primeros capítulos

Las primeras páginas, gratis — sin registrarse.

Esta muestra está en Kiswahili, el idioma en que está escrito el libro.

“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”

Mwanzo 1:27

Katika jambo la awali kabisa mwanamke kulifanya ni kujitambua. Wanawake wengi wameishi wakiwa hawajioni wao kuwa watu wa maana, imefika hatua ambayo wameanza kujishindanisha na wanaume. Wanapambana ili wajionyeshe kuwa wao ni bora tena ni bora sana kuliko wanaume. Ukishaanza kuona unapambana kushindana na mwanaume ujue shetani ameshakuweza. Mungu alipokuumba mwanamke alikuumba akiwa na kusudi na wewe, angetaka uzaliwe mwanaume asingeshindwa; ile kuzaliwa tu mwanamke kuna kazi amekuamini kwamba ni wewe utaifanya na sio mwanaume kwasababu hiyo kitendo cha kuanza kujifananisha na kujishindanisha na mwanaume ni ishara tosha haujui kwa nini umeumbwa mwanamke. Neno la Mungu lipowazi kabisa kwamba ‘Kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba’ sio mwanaume pekee aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hata sisi wanawake tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Ni fahari iliyoje kujua kuwa hata sisi wanawake ni sura na mfano wa Mungu. Tumeumbwa na kuitwa Adamu, sisi wote wanaume na wanawake ni binadamu hakuna sababu ya kujiona duni. Hata kubarikiwa hakubarikiwa mwanaume tu bali hata sisi wanawake ni wabarikiwa, Mungu alitubariki wote kwa pamoja. Neno la Mungu linasema “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.” - Mwanzo 5:1-2. Biblia inasema mwanamume na mwanamke aliwaumba akawabarikia, hakumbariki mmoja na kumuacha mwingine bali aliwabarikia kwa pamoja wote wana baraka za Mungu, kinachofurahisha zaidi ni Biblia inasema ‘akawaita jina lao Adamu’ hata jina tukaitwa Adamu, jina Hawa lilikuja baadaye kwasababu ya kazi ya uzao na hilo jina mwanamke alipewa na Adamu “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.” - Mwanzo 3:20. Mpaka sasa unaweza kuwa umeshaanza kuelewa kuwa ni uongo wa shetani wa kufanya wanawake wasijikubali na kujiona watu duni.

UMEUMBWA KWA NAMNA YA AJABU.

Jambo lingine ambalo limekuwa likisumbua wanawake wengi ni kutojikumbali muonekano wao, kitu ambacho kimepelekea kukosa kujiamini na kupoteza kufanya kile Mungu ameweka ndani yetu. Hii imepelekea wanawake kuhangaika sana na muonekano wa nje na kusahau kabisa kushughulika na mtu wa ndani. Sisemi kuhangaika na mtu wa nje ni jambo baya lakini hakikisha haichukui nafasi ya kuhangaika na mtu wako ndani. Mfano kupata muda wa maombi, kuhudhuria ibada, kusoma Neno la Mungu nk ni mambo ambayo yanamjenga na kumnawirisha mtu wa ndani. Pamoja na hayo wewe ni mzuri kwa namna ulivyoumbwa, iwe ni kimo mrefu au mfupi, iwe ni mnene au mwembamba, mweusi au mweupe kuna upekee na uzuri unao ambao hakuna mwanamke au mwanadamu mwingine anao. Wewe ni wa pekee kwenye kila kitu, shetani hutudanganya kuona hatufai nah ii huanza na kutusababishia katika kujifananisha na kujiringanisha na wengine. Mtunga Zaburi anaandika anasema “Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,” – Zaburi 139:13-

14. Mungu ametuumba kwa jinsi ya ‘ajabu na kutisha’ mwandishi wa zaburi hii anasema wazi kwamba ninakushukuru kwa kuwa nimeumbwa. Hivi ushawahi kumshukuru Mungu kwa kukuumba? Au ndio umeamini uongo wa shetani wa kukuonesha kuwa wewe ni mbaya, kwamba watu wanakuchukia sababu ya muonekano wako! Sio kweli wewe ni matokeo ya uumbaji wa Mungu wa ajabu na kutisha.

Hauna sababu ya kujichubua ngozi yako, hauna sababu ya kuvaa kiajabu au ki aibu. Biblia inaendelea kusema “Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.” - Zaburi 139:15-16. Kile kitendo umetoka tumboni mwa mama yako, ni matokeo ya Mungu kukuunga tangu ukingali tumboni, ustadi ulitumika lakini kinachofurahisha ni kwamba Mungu hakukuumba tu bali macho yake yalikuona kabla hujakamilika na akaziandika siku zako za kuishi kabla hazijawa bado. Unachopaswa kufanya ni kutambua wewe sio bahati mbaya, na upo hivyo ulivyo kwasababu kuna kusudi Mungu ameweka ndani yako. Wewe ni wa pekee, acha kuhangaika na uongo wa shetani. Usiwe kama Yeremia alisema kuwa yeye ni mtoto, wakati Mungu alimuweka kuwa nabii kabla hata hajazaliwa. “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.” – Yeremia 1:5-6. Mungu alijua kuwa Yeremia ni mtoto kama ambavyo anajua umbo lako lilivyo. Ila yeye haendeshwi na muonekano unaokusumbua bali anaendeshwa na kusudi lake aliloliweka ndani yako na hilo ndio wewe. Mwanamke jikubali, jipende na ujijali hivyo ulivyo kuna kazi nzuri Mungu ameweka ndani yako anataka uifanye na kuwa faida sio kwa familia yako na uzao wako tu bali uwe baraka kwa mataifa. Wala usijilinganishe na mtu mwingine kwa habari ya baraka wala usijisikie vibaya wengine wanapobarikiwa. Kila mmoja anawakati wake wa kujiliwa, wakati wako wa kubarikiwa upo njiani. Kumbuka Mungu amekuchora katika kitanga cha mkono wake kama anavyosema “Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.” - Isaya 49:17. Huna sababu ya kutembea umeinama, mwamini Mungu anakubariki na kukufanya baraka kwa wengine.

MWANAMKE KAMA MSAIDIZI.

Wanawake wengi hufikiri ile mwanamke kuitwa msaidizi inamaanisha yeye ni mtu duni, kwamba mwanaume anakuwa na thamani kubwa kuliko wao. Sio kweli, kuitwa msaidizi ni zao la mgawanyo wa kimajukumu ambao Mungu ameuweka yeye mwenyewe kwa mapenzi yake lakini kwa ajili yetu ili tuweze kufurahiana. Embu waza dunia yote ingekuwa ni wanaume tu, au dunia yote ingekuwa na wanawake peke yetu. Hakika isingevutia, wanaume na wanawake ndio wanaifanya dunia. Biblia inasema “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” – Mwanzo 2:18. Mungu anasema wazi kuwa msaidizi wa kufanana naye. Kwamba naye atakuwa ni mtu, naye ni mbarikiwa, naye lazima awe sura na mfano wa Mungu naye atatawala samaki wa majini, ndege wa angani, wanyama wa mwituni nk. Ukiviondoa hivyo anakuwa hajafanana na Adamu. Kuna wakati msaidizi anatakiwa kuwa na nguvu kuliko msaidiwa hivyo kuwa msaidizi haimaanishi kuwa mtu duni au kuwa wewe sio bora.

Kwa asili Mungu amemuumba mwanaume kuongoza familia. Kama umekuwa mdau wa mambo ya uongozi utakubaliana na mimi taasisi haiwezi kuongozwa na viongozi wawili lazima kuwe na kiongozi mmoja wengine watamsaidia hata kama wanaitwa viongozi. Nchi haiwezi kuwa na Rais wawili lazima itakuwa na Rais mmoja wengine watamsaidia. Ndivyo namna Mungu ameiweka ndoa kwamba Mwanaume atakuwa kiongozi na mwanamke atamsaidia. Kuna ndoa nyingi zinayumba na nyingine zimevunjika kwasababu tu mwanamke anapambana kuwa kiongozi kwa mume wake na kuiacha nafasi ya asili ya msaidizi ambayo Mungu aliiweka ndani yake. Mungu akupe neema kuifanya kazi yako kwa usahihi na ubora, kuna wakati shetani anataka kukutoa katika nafasi yako kwasababu ya vitu unavyopitia. Ila neema ya Mungu inakutosha kuhakikisha upo salama kwenye nafasi yako.

MWANAMKE NA KUZAA

Pamoja na kuwa msaidizi kuna mambo Mungu ameyaweka ndani ya mwanamke pekee na mwanaume hanayo, na kuna mambo Mungu ameyaweka kwa mwanaume peke yake mwanamke hana. Sasa ni muhimu kuyachochea na kuyatumia vyema yale yote ambayo Mungu ameweka ndani yako na kukufanya uwe wa pekee. Mungu amempa mwanamke tumbo la uzazi ambalo mwanaume hana. Mwanamke amepewa nguvu ya kuongeza, nguvu ya kuzidisha. Wewe ni mtu wa maana sana, ndio maana shetani anakutafuta kwa kila njia akumalize. Wewe ni mzalishaji kupitia wewe kuna vitu vikubwa vinazaliwa, kupitia wewe kuna mambo makubwa yatatokea katika ulimwengu. Yesu Kristo anapitia katika tumbo la mwanamke. Wewe ni njia nzuri ya kupitishia baraka. Hivi unajua hata katika familia kuna mambo mengi Mungu anayapitisha kupitia wewe? Funga milango ambayo shetani anaweza kuitumia kupenyeza vitu ambavyo si vya kiungu kwenye maisha yako. Funga milango inayoweza ondoa baraka za Mungu katika maisha yako. Usikubali shetani akutumie kufunga milango ya Baraka kwa maisha yako, kwa watoto wako, mume, ndugu taifa na kanisa.

Safari ya kuzaa huwa sio ya siku moja, mchakato wake huwa ni mrefu unahatua nyingi. Lakini kwa vile Mungu ameweka tumbo la uzazi ndani ya mwanamke basi kuzaa kutatokea tu, cha muhimu usiutupe mchakato. Kuitwa mama sio rahisi ila inawezekana kwasababu Mungu ameweka uwezo ndani yetu. Ameweka uwezo wa kuzaa na kuwa mama bora ndani ya nyumba mumeo akufurahie, watoto wakufurahie. Kuna wakati unafanya majukumu ya kuwa mama na hakuna anayetambua hiyo ni nafasi aliyokupa Mungu, ila tambua Mungu anakuona na anaitambua hiyo nafasi, pigana katika ulimwengu wa roho shetani asije akakufanya ukate tamaa. Kuna wakati maumivu uunayopitia yanakuwa makali sana, unakata tamaa, lakini usikate tamaa ipo siku mtoto atazaliwa, safari hii ni ndefu lakini iko siku kitu cha Ki-Mungu kitazaliwa, ipo siku utaona ndoto zikitimia katika maisha yako.

MWANAMKE NA UTUMISHI

Esto es aproximadamente el 62% de este capítulo. El resto continúa en el libro.

Comprar en Amazon ↗

“nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino..

Mwanzo 3:15

Katika kupigana vita vya aina yoyote ile, utakuwa wa ajabu unatuambia unapigana vita bila kujua adui unayepigana naye. Adui usiyemjua au usiyejua yupo wapi ni kazi ngumu kuishinda hiyo vita. Katika ulimwengu wa roho, sisi wanawake tayari tulishaambiwa, tulishajulishwa adui yetu ni nani. Mungu anauweka uadui kati ya nyoka - ibilisi na mwanamke ‘nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke’ mwanamke tambua mapema kabisa shetani sio rafiki yako, sio jirani yako, sio mtu wako wa karibu. Kamwe hatakuonea huruma, kamwe hatakuacha ufanikiwe kirahisi na hatakaa apende au kufurahia chochote kinachozaliwa sasa na hata kitakachozaliwa na wewe baadaye. Huu uadui ulianza pale bustanini na hautakaa ukome hadi Yesu atakaporudi, shetani ataendelea kupigana na mwanamke pamoja na uzao wake.

Mambo sio mepesi, pigana vita mwanamke wala usikate tamaa. Usipojiweka mkao wa kupigana vita ni lazima ujue kuwa shetani halali anapambana kukuweka kwenye himaya yake. Vita yake inafuatilia kizazi hadi kizazi. Yawezekana hata kwa kizazi chako vimeshaanza kupiga hodi. Yawezekana kuna vita umeshaviona umeanza kupambana. Kuna wakati mwanamke anabeba majukumu mazito sana ya watoto, kuwa mama na kuitunza familia, mambo ni mengi yanayomwagwa. Kama wanawake tusipojifunza kupigana vita vya kiroho ni ngumu sana kuona makusudi ya Mungu yanatimia kwa maisha yetu. Kama wewe ni binti unaona mambo ni magumu katika maisha yako, kama wewe ni mke unapoona kuna vita kwa ndoa yako, mambo ni magumu kazini, yote hiyo ni ishara kuwa upo kwenye uwanja wa mapambano unapaswa kupambana. Muhimu kujua hatupambani na hewa bali adui yetu shetani. Tusipopigana katika vita katika ulimwengu wa roho sisi tutakuwa ni watu wa kuhangaika sana katika ulimwengu wa mwili. Lakini punde utakapotambua kuwa uko vitani, utasimaama kama mwanamke ambaye anaijua nafasi yake.

Tofauti na hivyo utajikuta unapigana vita na watu wasiohusika bila kujua mleta vita ni shetani. Mungu akufungue macho uone na ujue huyo unayepambana naye sio aliyenyuma ya vita bali shetani ndio yumo nyuma yake.

UTAZAA KWA UCHUNGU.

Moja ya matokeo baada ya anguko la mwanadamu ambalo Mungu anamwambia mwanamke ni kwamba atazidisha uchungu wake katika kuzaa. “Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.” – Mwanzo 3:16. Yapo maumivu makali katika kumleta mtoto duniani, kwa wanawake ambao wamejifungua kwa njia ya kawaida wanawaeza wakaelewa zaidi kuhusu uchungu haswa muda ule unakaribia kujifungua. Uchungu mkali na wakati huo huo unatakiwa kumsukuma mtoto ili aweze kutoka. Wengi wakiwa kwenye hali hiyo walifikia hatua hata kusema sizai tena, lakini anapopewa mtoto na kumpakata kuna furaha moyoni kwamba nimepakata uzao wangu.

Kuna mchakato mrefu hadi mtoto anazaliwa tangu mwanamke alipobeba ujauzito. Kuna wengine huteseka tangu mwanzo mwa ujauzito hadi siku anajifungua. Huwa sio mchakato rahisi. Halikadharika kuna mambo mengi sana ili yazaliwe, ili hayo mambo yatokee kunaweza kuwa na maumivu kwa anayeyaleta mambo hayo au anayeyazaa mambo hayo. Kuna watu huwa wanawashangaa wanawake au wazazi ambao siku ya harusi hulia na kutoa machozi wanaposhuhudia watoto wao wakiingia kwenye ndoa. Ukweli ni kwamba mara nyingi huwa ni machozi ya furaha, machozi ya shukurani. Wakikumbuka Mungu alipomtoa huyo mtoto wanakosa maneno mazuri ya kusema. Kuna wanawake wamelea watoto peke yao kutokana na sababu mbalimbali. Wengine walitamani watoto wao wasikie hata sauti za baba zao lakini baba zao hawapo kwasababu mbalimbali. Mungu ni mwaminifu atakusaidia kuukuza uzao wako, pengine hiki kitabu kimekuja ili kukusaidia nini cha kufanya na uzao wako.

MWANAMKE MWENZAKO SIO ADUI YAKO.

Moja ya mbinu shetani hutumia kupigana ni hila, ametumia sana hila na kama hujagundua kuwa ni hila utajikuta umenasa kwenye mtego wake kama mwanamke. Hila moja wapo anayotumia ni kuhakikisha mwanamke anamchukia mwanamke mwenzake na anasahau kuwa mwanamke sio adui yake bali adui yake ni shetani. Nimeshuhudia wanawake kwa wanawake wakichukiana, wakisemana vibaya hata wale ambao wapo kanisani. Shetani kwa hila yake amefanya wanawake wawachukie wanawake wenzao kwa kiwango wapo wanawake wanasema siwezi kufanya biashara na mwanamke mwenzangu. Wengine wanasema siwezi kuwa na urafiki na mwanamke mwenzangu tutaishia kuwa wambea, ambacho wanakuwa hawajui ni kwamba wamekuwa wamenasa katika hila ya shetani. Hawa pale bustanini alidanganywa kwa hila na ibilisi, Mtume Paulo anawaandikia Wakoritho anasema “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.” 2 Wakoritho 11:3. Hila inaharibu fikira, namna tunawaza au kuyachukulia mambo. Hila inakufanya uache kuamini kilicho cha kweli na kuamini kingine ambacho ndio kibaya au hakina faida kwako. Shetani anatambua wanawake tukipendana, tukaungana na kuomba pamoja hatakaa kamwe utuweze.

Mwaka 2013 Mungu alinipa maono ya kuwa ninaandaa maombi ya wanawake. Kwamba wanawake kutoka sehemu mbalimbali, madhehebu mbalimbali tunakutana siku nzima tunaomba. Nilipojihakikishia kuwa ni jambo jema nikamshirikisha mchungaji wangu ambaye pia ni mume wangu, Mch Daktari Huruma Nkone. Mchungaji wangu alipoona ni jambo jema la kiungu akaniruhusu kuanza kufanya tukio hilo la maombi lijulikanalo kama ‘Ladies Prayer Weekend’. Wanawake tunakutana kwa pamoja huku tukijua sisi sio maadui, sisi ni wana wa Mungu na adui yetu ni shetani. Nimeshuhudia tukio hili la maombi likikua mwaka hata mwaka ki idadi lakini pia kimiujiza na matendo Mungu amekuwa akitendea wanawake wanaohudhuria tukio hili. Lilianza kama tukio dogo la kanisa la mahali lakini sasa sio tu wanawake wa kanisa la mahali wanaohudhuria bali wanawake kutoka makanisa na madhehebu mbalimbali ndani ya nchi nan je ya nchi. Kila ninapoona wanawake wanakutana pamoja katika maombi, katika biashara, katika malezi, katika mambo ya kiuongozi nk moyo wangu unafurahia kwasababu ninakuwa nimeona wanawake waliotambua kuwa mwanamke mwenzangu sio adui yangu bali ni mwanajeshi mwenzangu katika kumpinga adui yetu ibilisi.

MWANAUME SIO ADUI YAKO

Ukishaijua hila ya shetani ya kukufanya umchukie mwanamke mwenzako na ukavuka ukampenda basi ujue tu hataishia hapo. Shetani atakuja na hila nyingine ya kukuaminisha mwanaume ndio adui yako. Atakuletea mifano ya baadhi ya wanaume wanavyowatesa na kuwakandamiza wanawake, atakuonyesha baadhi ya wanaume wakiwasema vibaya na kuwadharau wanawake kisha anakuhitimishia kuwa mwanaume ndio adui wa mwanamke. Lakini ukweli mwanaume ni uzao wako mwanamke, ametoka katika tumbo lako, amekaa miezi tisa. Kila mwanaume unayemuona duniani ujue ni uzao wa mwanamke mwenzako. Huo uzao na wenyewe adui yao ni shetani, maana uadui wako na shetani unaenda hadi kwa uzao wako. Shetani anajua mwanaume na mwanamke wakiwa wamoja, wakawaza mazuri pamoja basi hana nafasi ya kuingia katika ndoa, katika familia na katika jamii kwa ujumla. Hivyo anachopambana ni kuhakikisha kwamba wanaume waone wanawake ndio adui yao na pia wanawake waone wanaume ndio adui yao.

Kwenye Biblia kuna habari ya mwanamke mmoja anaitwa Abigaili, mwanamke huyu aliolewa na mwanaume asiyefaa, asiye na sifa njema. Ingawa biblia haisemi ilikuwaje kuwaje Abigaili akaolewa na Nabali ila kwa haraka tungetarajia Abigaili kumchukia mumewe. Lakini naamini Abigaili alijua adui wake sio mumewe bali adui yake ni shetani. “Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake; naye alikuwa wa mbari ya Kalebu.” – 1 Samweli 25:3. Jaribu kuwaza mume wako hana adabu lakini pia ni mwovu. Habari inaendelea pale Nabali anawajibu vibaya watumishi wa Daudi na kugoma kabisa kuwasaidia. Daudi anadhamiria kumuangamiza Nabali, kwa bahati Abigaili anazipata taarifa anaamua kufanya jambo kumuokoa mume wake pamoja kwamba hafai, hana adabu na ni mwovu. “Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe Nabali, kasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu bwana wetu, naye akawatukana. Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda. Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.” – 1 Samweli 25:14,18,19,20. Abigaili anafanya kitendo cha kishujaa, anamjua mume wake, aliona hili tukilijadili na mume wangu sitoboi litazua balaa zaidi. Akaona ni heri ajaribu kulitatua kwa kwenda kuomba radhi badala ya mumewe. “Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi. Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako. Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.”

- 1 Samweli 25:23-24,28. Mwisho wa hi habari tunaona Nabali hakuangamizwa na Daudi kwasababu ya mwanamke mmoja aliyejua kusimama kwenye nafasi yake vyema hata kama mume wake alikuwa mwovu. Naamini alitambua adui sio mume wake, adui ni shetani.

HATUPASWI KUACHA KUZIJUA HILA ZAKE.

Esto es aproximadamente el 66% de este capítulo. El resto continúa en el libro.

Comprar en Amazon ↗