← Rudi
Vitabu

Majira ya Kuinuka

Tafakari

Mwaka wa kuinuka, wiki moja baada ya nyingine. Tafakari hii imejengwa juu ya dhamira kumi na mbili za kila mwezi na tafakari hamsini na mbili za kila wiki, ikianzia katika wito wa Abrahamu wa kuinuka na kuitembea nchi aliyoahidiwa. Kila wiki ina andiko, tafakari fupi, ungamo la imani na maombi — iliyoandikwa kusomwa kwa dakika chache na kubebwa siku zote zinazofuata.

TSh19,000 ≈ $8.99
Majira ya Kuinuka
Onjo la bure

Soma sura za mwanzo

Kurasa za kwanza, bure — bila kujisajili.

Andiko: “Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.” Mwanzo 13:17. KTafakari; atika Mwanzo 13:17 Mungu anamwambia Ibrahimu kuondoka na kutembea katika nchi aliyomuahidi atampa. Vivyo hivyo Mungu anakuita wewe kuinuka na kuziendea baraka zako alizokuandalia kwa maisha yako. Unaweza kujidharau au kujiona mnyonge lakini kumbuka Mungu yupo pamoja na wewe na ameshakupatia nchi ya kuimiliki. Unapotembea, tembea kifua mbele kwa imani, ataziongoza hatua zako na kukufikisha ndani ya ahadi zake. MAJIRA YA KUINUKA Ukiri wa Imani; Ninatangaza kwamba ninainuka na kumiliki zile ahadi Mungu amenipatia.

Hii ni takribani asilimia 67 ya sura hii. Sehemu iliyobaki inaendelea kitabuni.

Nunua Amazon ↗

Andiko: “(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)” 2 Wakoritho 5:7. KTafakari; utembea kwa imani maana yake ni kuwa na uhakika na ahadi za Mungu hata kama hauoni picha nzima ya jambo.Paulo anatukumbusha kwamba kumuamini Mungu kunapaswa kuongoza hatua zetu kuliko kuendeshwa na hofu au mazingira. Mambo yasiyotarajiwa yanapoibuka kumbuka kwamba Mungu anajua matokeo ya kila hatua tunayoipiga. Kaza macho yako kumuelekea yeye badala ya kuyatazama matatizo, na Mungu atakuongoza katika kusudi lake na kuzitimiza ahadi zake kwako. MAJIRA YA KUINUKA Ukiri wa Imani; Ninatangaza na kukiri kwamba nitatembea kwa imani na si kwa kuona

Hii ni takribani asilimia 69 ya sura hii. Sehemu iliyobaki inaendelea kitabuni.

Nunua Amazon ↗

Kuingia katika Ardhi Eneo lako Mungu alilokupatia. Andiko: “Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.” Yoshua 1:3. MTafakari; ungu anamhakikishia Yoshua kwamba kila eneo tunalolikanyaga ni eneo la Mungu. Hii ahadi inamaana kwamba kila unapoinuka kila siku, Mungu anakuwa ameshaandaa baraka katika njia yako. Unaweza kusonga mbele ukiwa na uhakika kwamba hilo eneo umekanyaga Mungu amekumilikisha. Inuka ukiwa na mamlaka na udai ahadi zako, kwani kwa jambo jema kuna ahadi ya Mungu kwa ajili yako. Tembea kwa ujasiri kila siku, kwa uhakika kwamba ardhi unayoikanyaga ni zawadi ya Mungu kwako. MAJIRA YA KUINUKA Ukiri wa Imani; Ninatangaza kwamba nitatembea katika ardhi Mungu aliyoniahidia.

Hii ni takribani asilimia 70 ya sura hii. Sehemu iliyobaki inaendelea kitabuni.

Nunua Amazon ↗

Nihuishe nguvu zangu kuziomba Ahadi za Mungu. Andiko: “bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai;….” Isaya 40:31. KTafakari; una nyakati safari huwa ndefu na ya kuchosha, lakini ahadi ya Mungu katika kumgojea huambatana na kuhuisha nguvu zetu. Unapoinuka kila siku kutekeleza mapenzi ya Mungu, Nguvu zake hutuinua zaidi ya kila changamoto tunazokutana nazo. Hata katikati ya uchovu mwingi, Roho wake hutuhuisha. Amini kwa majira na wakati wake tutapaa juu kwa mbawa kama tai na kumaliza mbio salama. Amini kwamba nguvu za Mungu ni sahihi kabisa katikati ya udhaifu wako unapoendelea mbele kwa imani. MAJIRA YA KUINUKA Ukiri wa Imani. Ninatangaza kwamba ninahuishwa nguvu zangu katika Bwana.

Hii ni takribani asilimia 71 ya sura hii. Sehemu iliyobaki inaendelea kitabuni.

Nunua Amazon ↗